November 10, 2023

Wadau wa uziduaji wameshauri baadhi ya vipengele vya Sheria ya Madini ya mwaka 2017 kufanyiwa marekebisho, ili kuongeza ufanisi katika sekta ya madini. Wametoa wito huo leo Novemba 9,2023 katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Uziduaji, lililoandaliwa na Shirikia lisilo la kiserikali la HakiRasili...

Wadau wa uziduaji wameshauri baadhi ya vipengele vya Sheria ya Madini ya mwaka 2017 kufanyiwa marekebisho
Wadau wa uziduaji wameshauri baadhi ya vipengele vya Sheria ya Madini ya mwaka 2017 kufanyiwa marekebisho, ili kuongeza ufanisi katika sekta ya madini. Wametoa wito huo leo Novemba 9,2023 katika mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Uziduaji, lililoandaliwa na Shirikia lisilo la kiserikali la HakiRasilimali, kwa lengo la kujadili mafanikio na changamoto katika sekta ya madini, pamoja na kutoa mapendekezo ya maboresho.

Kwa mujibu wa wadau hao, mojawapo ya kipengele cha sheria ni kile kinacholazimisha makampuni ya uchimbaji madini ya nje kuwa na akaunti ya Benki nchini (Tanzania) tu, hatua inayowakosesha mitaji ya uzalishaji madini. "Uchimbaji madini unahitaji mitaji mkubwa ambayo taasisi zetu za ndani za kifedha bado hazijawa na uwezo wa kukopesha. "Kwa mfano, uzalishaji wa madini ya Nikeli katika mgodi wa Kabanga unahitaji takribani dola za kimarekani billioni moja, kiasi ambacho upatikanaji wake kwa benki za nchini ni changamoto," amesema Meneja Mkuu wa Kampuni ya Adavale Resources (TZ) Limited, Gerald Mturi. Mwisho

Related Posts

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi) 2026
Jul 21, 2026

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi) 2026

About the Programme ESKi Tanzania is a capacity development programme designed to nurture and empower the next generation of leaders, community advoca...

CALL FOR ABSTRACTS
Jun 12, 2026

CALL FOR ABSTRACTS

📢 CALL FOR ABSTRACTS HakiRasilimali invites researchers, academics, practitioners, policymakers, and civil society actors to submit abstracts for th...

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 02, 2025

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

ESKi Tanzania ni programu ya kukuza uwezo iliyoundwa ili kukuza na kuendeleza kizazi kipya cha viongozi, watetezi wa jamii na wataalamu wanaoshughulik...