November 06, 2024

Dodoma, Tanzania – Novemba 5, 2024 Naibu Waziri Mkuu, Dk. Doto Biteko, amesisitiza azma ya Tanzania katika kutumia rasilimali zake kwa njia endelevu ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, zinazosababishwa na matumizi ya nishati chafu. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Uziduaji.....

Dk. Biteko Atoa Mwelekeo wa Matumizi ya Nishati Safi Nchini Tanzania
Dodoma, Tanzania – Novemba 5, 2024

Naibu Waziri Mkuu, Dk. Doto Biteko, amesisitiza azma ya Tanzania katika kutumia rasilimali zake kwa njia endelevu ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, zinazosababishwa na matumizi ya nishati chafu. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Uziduaji linaloendelea jijini Dodoma kwa siku mbili, Dk. Biteko alieleza kuwa mwelekeo wa dunia sasa ni kuelekea matumizi ya nishati safi, na Tanzania ipo tayari kushiriki kikamilifu katika kampeni hiyo.

Dk. Biteko alisema kuwa Tanzania ina akiba kubwa ya gesi asilia, ikiwa na ugunduzi wa futi za ujazo trilioni 57.54, ambapo trilioni 47.4 zimegunduliwa katika eneo la kina kirefu cha bahari na trilioni 10.12 kwenye maeneo mengine. Alifafanua kuwa rasilimali hii ya gesi asilia ni fursa muhimu kwa nchi wakati huu ambapo dunia inaelekea kwenye matumizi ya nishati safi. "Ugunduzi wa gesi ni fursa kubwa kwetu katika harakati hizi za mabadiliko ya nishati kwani changamoto kubwa zinazoikumba dunia sasa ni mabadiliko ya tabianchi," alisema Dk. Biteko.

Zaidi ya watu 200 kutoka mataifa manne tofauti walihudhuria jukwaa hilo, ambapo mada mbalimbali ziliangazia mwelekeo wa Tanzania katika kukuza matumizi ya nishati safi, hususan gesi asilia. Hata hivyo, Dk. Biteko alikumbusha umuhimu wa kuzingatia hali halisi ya kiuchumi wa wananchi kwani, kwa sasa, matumizi ya nishati safi ni ya gharama kubwa ikilinganishwa na nishati nyingine zinazotumika. "Nishati safi tunaihitaji sana, lakini tutaendelea kutumia nishati nyinginezo hususani kwa ajili ya upatikanaji wa umeme. Tunahitaji kuleta maendeleo na kubadili maisha ya wananchi wetu," alihitimisha Dk. Biteko.

Related Posts

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 02, 2025

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

ESKi Tanzania ni programu ya kukuza uwezo iliyoundwa ili kukuza na kuendeleza kizazi kipya cha viongozi, watetezi wa jamii na wataalamu wanaoshughulik...

Call for Application – Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 01, 2025

Call for Application – Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

Capacity-building opportunity for CSOs, youth and media to deepen technical expertise.

External audit services tender
Aug 14, 2025

External audit services tender

HakiRasilimali invites qualified firms to submit proposals for annual audit engagements.