October 23, 2021

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema ofisi ya Bunge itaendelea kushirikiana na asasi za kiraia katika mazingira rafiki, huru, wazi, na sawa ili kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa huku akizitaka kurekebishana kwa zile zinazoenda tofauti. Ndugai amesema hayo Oktoba 23, 2021 wakati akizu.....

Bunge Kuendeleza Ushirikiano na AZAKI
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema ofisi ya Bunge itaendelea kushirikiana na asasi za kiraia katika mazingira rafiki, huru, wazi, na sawa ili kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa huku akizitaka kurekebishana kwa zile zinazoenda tofauti.

Ndugai amesema hayo Oktoba 23, 2021 wakati akizungumza katika maonyesho ya wiki ya Azaki 2021 ambapo yeye alihudhuria kama Mgeni rasmi. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Azaki na maendeleo.

“Natambua kwamba Bunge na Azaki ni wadau muhimu katika utendaji wa kazi hasa katika sera, sheria, bajeti, na masuala mbalimbali yanayowahusu wananchi, kuna mahali ambapo Serikali wakati mwingine haifiki lakini Azaki zinafika,” amesema Ndugai.

Hata hivyo amesema licha ya kazi kubwa inayofanywa na baadhi ya asasi za kiraia, zipo ambazo hazifanyi kazi vizuri ndiyo maana zilitungwa sheria mbalimbali za kudhibiti endapo mapengo yataonekana.

Related Posts

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi) 2026
Jul 21, 2026

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi) 2026

About the Programme ESKi Tanzania is a capacity development programme designed to nurture and empower the next generation of leaders, community advoca...

CALL FOR ABSTRACTS
Jun 12, 2026

CALL FOR ABSTRACTS

📢 CALL FOR ABSTRACTS HakiRasilimali invites researchers, academics, practitioners, policymakers, and civil society actors to submit abstracts for th...

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)
Sep 02, 2025

Call for Application-Extractive Sector Knowledge Transfer Incubator (ESKi)

ESKi Tanzania ni programu ya kukuza uwezo iliyoundwa ili kukuza na kuendeleza kizazi kipya cha viongozi, watetezi wa jamii na wataalamu wanaoshughulik...