Mkurugenzi wa Taasisi ya HakiRasilimali Adam Anthony “Wananchi wanapaswa kufurahia uwepo wa rasilimali katika maeneo yao. Anthony aliyasema hayo Novemba 05, 2024 wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la uziduaji mwaka 2024 linaloendelea kwa siku mbili jijini Dodoma, na wadau wa sekta hiyo kutoka mataifa manne tofauti.
Naibu Waziri Mkuu Doto Biteko ndiye aliyelizindua Jukwaa hilo kwa mwaka huu mada kuu ni kuwezesha maendeleo endelevu ndani ya sekta uziduaji lakini pia masuala yahusuyo manufaa ya wananchi, ushiriki wa makundi tofauti na mazingira kwa ujumla. Akitoa neno la ufunguzi Anthony alianza kwa kuelezea shughuli za taasisisi ya HakiRasilimali huku akisisitiza kuwa ina imani katika uwazi na ni chachu ya maendeleo ya sekta ya uziduaji. “Sekta ya uziduaji ni ya muhimu kwa Taifa na ninapongeza hatua za kisera zinazofanywa na Serikali, ni muhimu kwani wananchi wanapaswa kufurahia rasimali hizo” Aidha ameahidi kuwa HakiRasilimali itaendelea kushirikiana na wadau wote wanaoleta maendeleo katika sekta hiyo, akisisitiza kuwa uwazi chachu ya uwajibikaji.
Share This Story, Choose Your Platform!
continue reading
Related Posts
Wadau wa sekta ya uziduaji waishauri serikali kuweka mikakati thabiti
Msimamizi wa kitengo cha Biashara katika Kituo cha Sheria na
Dodoma, Tanzania. Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alifunga rasmi Jukwaa