Karibu katika toleo la sita la DARUBINI, Toleo hili la DARUBINI linasisitiza umuhimu wa majukwaa ya kimataifa yenye mjumuiko wa wadau mbalimbali hasa katika majadiliano yanayohusu miongozo ya kiuwajibikaji katika upatikanaji wa rasilimali ambayo ni suluhu katika changamoto za haki za binadamu, athari za kimazingira.Toleo hili limeangazia kwa kina hasa ushiriki wa serikali katika kupelekea na kuchochea miongozo, kanuni na viwango vya uwajibikaji katika mnyororo wa ugavi wa madini. Vilevile toleo hili limejumuisha sauti za jamii zinazo ibua na kutoa picha halisi kuhusu masuala ya haki za binadamu katika shughuli zinazo fanyika ndani ya sekta ya uziduaji.