Mwaka 2017 Bunge la Tanzania lilipitisha Miswada ya Sheria ya ulinzi wa Rasilimali za Taifa.
Sheria hizo zililenga kudhibiti usafirishaji wa Rasilimali ghafi (madini) nje ya nchi yakiwamo maarufu kama makinikia kwa ajili ya uchakataji. Pia, sheria hizo zilibadilisha viwango vya Tozo mfano Mrabaha ulipanda kutoka asilimia 3 mpaka 6 lengo likiwa kuongeza mapato ya Serikali.
Sheria hizo pia zilitoa mamlaka kwa serikali kupata asilimia 16 za hisa kutoka kwenye kila kampuni ya uchimbaji mkubwa wa madini.
Kesho kwenye mjadala wa Mamlaka ya kudumu na uwekezaji katika sekta ya uziduaji tutasikiliza mjadala huo ulioandaliwa na taasisi ya HakiRasilimali katika hoteli ya Royal Village jijini Dodoma, ambapo atakuwepo waziri wa Madini, Mhe. Dotto Biteko, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato, na Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhe. Exaud Silaoneka.