By |Published On: January 23, 2025|

Sekta ya Uchimbaji Mdogo Tanzania ni moja ya sekta inayochangia vyema kiuchumi, kuimarisha pato la wachimbaji na Maisha yao ikiwemo wanawake wengi waliopo kwenye sekta hii. Licha ya mchango wao katika Sekta hii wanawake wengi wameendelea kupitia changamoto za ufinyu wa fursa zilizopo katika sekta ya madini na hivyo kupelekea kukosekana kwa usawa wa kushiriki katika fursa za kiuchumi. Vikwazo vya kimfumo ikiwemo mila na desturi kandamizi zinazolenga kuzuia ushiriki ukamilifu wa wanawake katika kumiliki leseni za uchimbaji wa madini, kupata mikopo ya fedha na vifaa, taarifa ya kijielojia Pamoja na kukosekana kwa vifaa vya kisasa katika uchimbaji na uchenjuaji wa madini vinamkwamisha mwanamke kukua kiuchmi katika sekta ya madini.

Mgodi wa Ntabalale, unalenga kupambana na changamoto za kijinsia kwa wanawake walio sehemu za ajira za mgodi Pamoja na wanaoshiriki katika shughuli mahala pa kazi. Lengo ikiwa ni kupunguza vikwazo vya usawa wa kijinsia na kutambua mchango wa mwanamke katika shughuli za uchimbaji.

Kulingana na mfumo wa uchimbaji mdogo kuwa na ajira ndogo ndogo kwa wingi mahala pa kazi, ni muhimu kusisitiza juu ya kuimarisha mfumo wa usawa wa kijinsia. Na kutokana na mfumo wa uchimbaji kuwa na waajiriwa wengi wa jinsia ya Me mahali pa kazi Mfano sehemu ya maduara ambapo shughuli nyingi zinafanyawa na wanaume na sio jinsia ya Ke kulingana na aina ya kazi na nguvu inayohitajika katika kufanya kazi hiyo.

Sera hii inalenga kupunguza na kuondoa kabisa ubaguzi wa kijinsia na kuchochea usawa wa kijinsia mahala pa kazi na kulenga kuwezesha wanawake kupata usawa wa fursa zilizopo katika sekta ya madini. Ikiwemo kuondosha mila na desturi kandangamizi zinazolenga kumkandamiza mwanamke mahala pa kazi. Vilevile sera hii inalenga kuondosha ubaguzi na unyanyasi wa kijinsia wa wanawake kwa lengo la kuboresha nafasi ya mwanamke katika kushiriki shughuli za kiuchumi na kufanya maamuzi yanayohusiana na kazi au binafsi mahala pa kazi pamoja na kuheshimu mawazo yao.