Tanzania inajulikana kama taifa lenye utajiri mkubwa wa maliasili, hasa katika sekta ya ya uziduaji. Ahadi ya ustawi wa kiuchumi, imeunganishwa dhidi ya ukweli
dhahiri wa mapambano juu ya kupata suluhu hasa pale shughuli za uchimbaji wa rasilimali zinapoleta madhara kwa watu au mazingira. Kwa jamii zilizoathiriwa moja kwa moja na shughuli za uziduaji, kutafuta haki kunaweza kuhisiwa kama ni changamoto isiyoweza kutatuliwa. Makala hii inaangazia matatizo yanayowakabili Watoa Msaada wa Kisheria nchini Tanzania wanapopitia sheria na sera tata zinazo ongoza na kutawala sekta ya uziduaji, kwa lengo la kutoa misaada ya kisheria kwa waathiriwa wa sekta ya uziduaji