WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde, ametaja mikakati ya Wizara hiyo katika kuikuza Sekta ya madini kiuchumi ifikapo 2030 kwa kuwekeza kwanza kwenye utafiti. @wizara_ya_madini_tanzania Amebainisha hayo wakati akihitimisha Jukwaa la Sekta ya Uziduaji yani Madini, Mafuta na Gesi Asilia ambalo limefanyika kwa muda wa Siku Mbili Jijini Dodoma lililoandaliwa na Taasisi ya HakiRasilimali.
Amesema baada ya Rais Samia kumteua kuwa Waziri wa Madini, aliangalia Sekta ya Madini, Sera ya Madini ya mwaka 2009 na kufuata maelekezo ya CCM kupitia Ilani ya uchaguzi, na maelekezo ya viongozi wakubwa akiwamo Mheshimiwa Rais, kuona namna ya kuikuza Sekta hiyo na kuchangia uchumi wa nchi kwa kiwango kikubwa.
Amesema wao kama Wizara ya Madini pamoja na viongozi wenzake walikuja na jambo la Vission 2030 yani Madini ni Maisha na Utajiri, na kujiwekea malengo kwamba hadi ifikapo mwaka huo 2030 kwamba nchi ya Tanzania kupitia Sekta ya Madini wawe wamefanya utafiti wa kina wa Madini tuliyonayo ifikie asilimia 50 na kutoka asilimia 16. “Moja kati ya Changamoto kubwa tuliyonayo hapa Nchini ni kutokuwa na Taarifa sahihi ya Madini tuliyonayo, hivyo tukaona sehemu ya kwanza ya kuanzia tuanzie hapa, na njia ya pekee ni kuipa nguvu GST ili waweze kuwa na uwezo wa kufanya kazi zake kwa mujibu wa Sheria, na lengo letu ni kuimarisha Kanzidata yetu kupitia utafiti wa ‘Georgyical’ Sayansi, na kuongoza wadau wa Sekta ya madini vizuri,”amesema Mavunde.
Aidha,amesema kama Wizara waliona ni vyema waweke mikakati ya kuhakikisha wanafanya utafiti wa kina na kulifikia eneo kubwa zaidi la madini, na kubainisha kuwa kama eneo tu hilo dogo ambalo limefanyiwa utafiti wa kina wa madini kwamba linaingizia mapato mengi Serikali Je eneo hilo kubwa itakuwaje, ndiyo maana kwa sasa wapo kwenye utafiti ili kupata taarifa sahihi ya madini. “Eneo hilo dogo tu ambalo limefanyiwa utafiti wa kina wa madini tuliyonayo limekuwa na mchango mkubwa wa mauzo ya madini nje ya nchi, ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita yamefikia kiasi cha Dola Bilioni 3.3 sawa na asilimia 56 ya mauzo yote ya bidhaa nje ya nchi, huku Serikali kuu ikikusanya Maduhuli Bilioni 878, na Mapato ya Kodi ya ndani kiasi kilichokusanywa ni Sh.Trilioni 2,”

Share This Story, Choose Your Platform!

continue reading

Related Posts