Dodoma, Tanzania.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alifunga rasmi Jukwaa la Uziduaji kwa mwaka 2024, huku akisisitiza maoni ya wadau mbalimbali ni muhimu katika kuiiendeleza sekta ya Madini,aliipongeza HakiRasilimali kwa kuanda jukwaa hilo ambalo limehudhuriwa na wadau kutoka maeneo tofauti ndani na nje ya nchi.
“Kusanyiko kama hili linatupa nafasi sisi kama Serikali kupata mawazo na mbinu mbalimbali za kuendeleza sekta ya madini,Niwahakikishie, yale maazimio yote tisa mliyojadili kwenye jukwaa hili tumeyachuka na tunayafanyia kazi,” alisema.
Aidha Mavunde ameweka wazi kuwa Serikali ina mpango endelevu wa kuwawezesha kina mama na vijana katika sekta ya madini.
“Tayari tumefuta leseni zaidi ya 6248 kwa watu waliokuwa wanamiliki maeneo makubwa yenye rasilimali bila kuyatumia na sasa tumeyarudisha serikalini na tuna mpango wa kuyatoa kwa kina mama na vijana wa kitanzania kwaajili ya kuyafanyia kazi,tuna mipango ya kuhakikisha kina mama katika sekta ya uziduaji wananufaika. Tupo kwenye hatua nzuri, tumekaa na wadau mbalimbali na tumeanza kuona matunda yake. Miongoni mwake ni mikopo ya fedha,vifaa na mambo mengine yanayohitajika,” alisema.
Wakati huo huo, Mavunde aliwaomba watanzania kujivunia maendeleo yanayotokea kwenye sekta ya madini kwani ilivyokuwa mwanzo ni tofauti na sasa.
“Kabla ya mabadiliko ya sheria ya mwaka 2017 vifungu 102, 105 vya madini mambo yalikuwa magumu kwa jamii kunufaika na migodi iliyowazunguka lakini kwa sasa mambo yamebadilika na wanajamii waliopo maeneo ya migodi wananufaika.Pia watanzania wamepata ajira kwenye migodi mikubwa na nafasi zile za juu sasa wapo watanzania wengi. Kwa miaka hii mitatu zaidi ya ajira 17633 za moja kwa moja zimetolewa kwa watanzania huko migodini”
“Tunaendelea kujenga viwanda kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuwawezesha wananchi na kuhakikisha vifaa na machine zinazotumika migodini zizalishwe hapa hapa na fedha yetu ibaki hapa nchini kuliko kuagiza kila kitu nje ya nchi.”
Pia Mavunde alikiri kuwepo kwa changamoto katika ulipaji wa fidia sambamba na mkanganyiko wa sheria ya aridhi na kuweka wazi kuwa ataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutafuta suluhu.
Eneo lingine ambalo Mavunde alizungumzia ni kwenye matumizi ya Zebaki na mipango ya Serikali kwenye madini mkakati.
“Ni kweli tuna changamoto huku kwenye matumizi ya Zebaki. Ila tumeanzisha vituo vitatu vya mafunzo kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo kutoka kwenye matumizi ya zebaki na kutumia mitambo ya kisasa.,” alisema Mavunde na kuongeza;
“Tanzania ni kati ya nchi chache zenye neema ya madini ya mkakati. Tunaanda mikakati maalumu ya kuyavuna. Sitatoa leseni nyingine kubwa kwa kampuni yetote kama haitakuja na mpango mzuri wa namna ya kuongeza thamani madini mkakati ndani ya nchi. Ni muda mwafaka sasa kwa watanzania kunufaika na madini haya mkakati.”
Share This Story, Choose Your Platform!
continue reading
Related Posts
Wadau wa sekta ya uziduaji waishauri serikali kuweka mikakati thabiti
Msimamizi wa kitengo cha Biashara katika Kituo cha Sheria na
Dodoma, Tanzania – Novemba 5, 2024 Naibu Waziri Mkuu, Dk.