Msimamizi wa kitengo cha Biashara katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Joyce Komanya alitaja maeneo matatu ya kuwasaidia waathirika wa changamoto mbalimbali katika sekta ya uziduaji kupata nafuu, ikiwa ni pamoja na mifumo ya kimahakama na mifumo ya kiserikali isiyokuwa ya kimahakama.
Komanya alieleza hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu upatikanaji wa nafuu kutoka kwenye changamoto katika sekta ya uziduaji, kwenye Jukwaa la Uziduaji 2024 lililofanyika Dodoma siku mbili mfululizo.
Alisema katika upatikanaji wa nafuu kwenye sheria na haki za binadamu njia ya kwanza inayotumika ni ya kisheria ambayo huwasaidia waathirika katika masuala ya uvunjifu wa amani kwenye biashara.
” Kesi nyingi ni za masuala ya haki za ajira, kesi za ardhi na uchafuzi wa mazingira na kwenye ardhi nyingi ni kesi za umiliki wa ardhi” alisema Komanya.
Eneo lingine ni mifumo ya kiserikali isiyokuwa ya kimahakama inayotumika kutatua migogoro ambapo malalamiko yanayohusiana na sekta ya uziduaji yanaweza kupelekwa katika Tume ya Uchimbaji, Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwenye kesi zinazohusu uchafuzi wa mazingira.
“Pia, kuna Tume ya Uamuzi na Usuluhishi (CMA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) ambazo kuna sheria inayozielekeza mamla hizi kusikiliza malalamiko na kuwapatia nafuu waathirika, ” alisema.
Alitaja eneo la tatu kuwa ni mifumo iliyowekwa na makampuni yaliyo katika sekta ya uziduaji kushughulikia malalamiko na migogoro inayotokea kwenye maeneo yao ili kuitatua.
Share This Story, Choose Your Platform!
continue reading
Related Posts
Wadau wa sekta ya uziduaji waishauri serikali kuweka mikakati thabiti
Dodoma, Tanzania. Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alifunga rasmi Jukwaa
Dodoma, Tanzania – Novemba 5, 2024 Naibu Waziri Mkuu, Dk.