Wadau wa sekta ya uziduaji waishauri serikali kuweka mikakati thabiti ya kisera na kisheria ili kuhakikisha rasilimali za madini hasa ya madini kimkakati yananufaisha watanzania.Huku takwimu zikionesha mwaka 2022, sekta ya uziduaji ilichangia asilimia 9.1% katika Pato la Taifa na ilichangia zaidi ya 40% ya mauzo ya nje.

Akizungumza katika jukwaa la uziduaji mwaka 2024 lililofanyika Dodoma , muhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam , Profesa Abel Kinyondo alisema iko haja yua kufanya mapitio yua kuangalia ni kwa namna gani sera na sheria zinatekelezwa ili kuhakikisha madini ya kimkakati yanakuwa na manufaa zaidi kwa watanzania.

“Tuna tunga sheria na tunakua na sera lakini je tumewahi kukaa chini kujadili hizo sheria na sera zilizopo tunatekeleza kwa kiwango gani kuangalia madhara ya mikataba ya nyuma katika uwekezaji ili kuhakisha rasilimali hizi zinanufaisha watanzania,”alisema.

Suala la utunzaji mazingira hususani katika shughuli za uziduaji ni moja ya mada ambayo ilijadiliwa katika jukwaa hilo,ambapo akiangazia suala la kufuata sheria katika suala la utunzaji mazingira hususani katika shughuli za uziduaji,Meneja mkuu katika kampuni ya Adavale Resource , Bw Gerald Mturi amesema kwa kiasi kikubwa makampuni yaliyowekeza katika sekta ya uziduaji yamekua ya kizingatia sheria na kanuni ili kulinda mazingira.

Jukwaa la uziduaji la mwaka huu lilihudhuriwa na wadau mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo DRC,Kenya na Uganda4

Share This Story, Choose Your Platform!

continue reading

Related Posts