Siku chache zilizopita, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli aliunda kamati mbili za wataalamu kwa ajili ya kuchunguza taarifa za kuwapo kwa udanganyifu wa kiwango cha madini katika mchanga wa dhahabu (makinikia), ambao umekuwa ukisafirishwa kupelekwa nje ya nchi. Mchanga huo ni ule unaotoka katika migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi ambayo kwa pamoja inamilikiwa na Kampuni ya Acacia.

Kamati hizo pia zilipewa kazi ya kutoa mapendekezo kuhusu namna bora ya kusimamia sekta ndogo ya madini ya dhahabu. Zaidi ya hapo, kamati hizo pia zilitakiwa kuchunguza na kuchambua masuala ya fedha katika shughuli za uchimbaji wa madini nchini. Matokeo ya uchunguzi wa kamati hizo, yalizaa kikao baina ya Rais Magufuli na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick (ambao ni wamiliki wa sehemu kubwa ya Acacia), Profesa John P. Thornton, hatua ambayo imefungua milango ya majadiliano baina ya wawekezaji hao na serikali ya Tanzania.

Baada ya kufuatilia kwa umakini mkubwa matukio haya pamoja na mwitikio wa jamii kuhusu hatua zilizochukuliwa, Jukwaa la Asasi za Kiraia la HakiRasilimali – PWYP tunaofanya kazi ya utetezi katika sekta ya madini, yenye wanachama tajwa hapo chini tunapenda kueleza msimamo wetu.

Tumefanya mapitio ya mihtasari ya taarifa zote mbili tunaunga mkono baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na kamati ambayo yanajenga msingi wa hoja zilizokuwapo tangu mwanzo, hivyo tutapenda kueleza mtazamo wetu.

soma zaidi:HAKIRASILIMALIPWYPTAMKO

 

Imeandaliwa na:

Sekretarieti ya HakiRasilimali – PWYP

Muhimu: HakiRasilimali ni jukwaa la Asasi za Kijamii (CSOs) ambazo zimesajiliwa kama kampuni zisizotengeneza faida chini ya Sheria ya Kampuni ya 2002 ambazo zinafanya kazi mahususi kuhusu masuala ya madini, mafuta na gesi nchini Tanzania. HakiRasilimali ni taasisi mshirika wa Publish What You Pay (PWYP), ambayo inaundwa na wanachama ambao ni muungano wa asasi za kiraia katika nchi zaidi ya 40 duniani kote. Lengo la asasi hizo ni kuhimiza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya rasilimali za madini, mafuta na gesi.

(Wanachama: Action for Democracy and Local Governance, Governance Links, Governance and Economic Policy Centre, Interfaith Standing committee, ONGEA, HakiMadini, Policy Forum, Tanganyika Law Society).