DODOMA: Kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini imeshauri wadau katika sekta ya uziduaji kufikiria teknolojia mpya itakayowawezesha wachimbaji wadogo kuepukana na matumizi ya zebaki katika uchimbaji wa dhahabu. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, David Mathayo katika jukwaa la uziduaji 2024 linalofanyika Dodoma tarehe 5 na 6 Novemba, 2024. Jukwaa hilo ambalo limeratibiwa na HakiRasimali na kuzinduliwa na Naibu Waziri Mkuu Dkt.Doto Mashaka Biteko linalenga kujadili na kubadilisha uzoefu miongoni mwa wadau katika sekta ya uziduaji nchini ambayo inajumuisha madini, mafuta na gesi. Mr Mathayo amesema zebaki imekua ikitumika na wachimbaji wadogo katika kuchimba dhahabu kutokana na kukosa njia mbadala jambo ambao limekua likiathiri pakubwa afya za wachimbaji hao.
Amesema matumizi ya teknolojia bora yatawezesha kulinda afya za wachimbaji pamoja na kuongeza uzalishaji. “Hili ni tatizo kubwa ambalo madhara yake kila mmoja anatambua, hata wanaotumia wenyewe wanajua, tunaomba tuendelee kuongeza teknolojia na kuweza kuangalia namna bora zaidi ya kupata dhahabu bila kutumia zebaki,”amesema. Hata hivyo ameiomba serikali kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa kuwapa mitaji huku akisisitiza kuwa wachimbaji hao ambao wako kwa asilimia 40 wamekua na mchango mkubwa katika kuongeza pato la taifa. Jukwaa la uziduaji la mwaka huu limeudhuriwa na wadau kutoka mataifa mbali mbali ikiwemo DRC,Kenya na Uganda.
Share This Story, Choose Your Platform!
continue reading
Related Posts
Wadau wa sekta ya uziduaji waishauri serikali kuweka mikakati thabiti […]
Msimamizi wa kitengo cha Biashara katika Kituo cha Sheria na […]
Dodoma, Tanzania. Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alifunga rasmi Jukwaa […]