Dodoma, Tanzania – Novemba 5, 2024
Naibu Waziri Mkuu, Dk. Doto Biteko, amesisitiza azma ya Tanzania katika kutumia rasilimali zake kwa njia endelevu ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, zinazosababishwa na matumizi ya nishati chafu. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Uziduaji linaloendelea jijini Dodoma kwa siku mbili, Dk. Biteko alieleza kuwa mwelekeo wa dunia sasa ni kuelekea matumizi ya nishati safi, na Tanzania ipo tayari kushiriki kikamilifu katika kampeni hiyo.
Dk. Biteko alisema kuwa Tanzania ina akiba kubwa ya gesi asilia, ikiwa na ugunduzi wa futi za ujazo trilioni 57.54, ambapo trilioni 47.4 zimegunduliwa katika eneo la kina kirefu cha bahari na trilioni 10.12 kwenye maeneo mengine. Alifafanua kuwa rasilimali hii ya gesi asilia ni fursa muhimu kwa nchi wakati huu ambapo dunia inaelekea kwenye matumizi ya nishati safi. “Ugunduzi wa gesi ni fursa kubwa kwetu katika harakati hizi za mabadiliko ya nishati kwani changamoto kubwa zinazoikumba dunia sasa ni mabadiliko ya tabianchi,” alisema Dk. Biteko.
Zaidi ya watu 200 kutoka mataifa manne tofauti walihudhuria jukwaa hilo, ambapo mada mbalimbali ziliangazia mwelekeo wa Tanzania katika kukuza matumizi ya nishati safi, hususan gesi asilia. Hata hivyo, Dk. Biteko alikumbusha umuhimu wa kuzingatia hali halisi ya kiuchumi wa wananchi kwani, kwa sasa, matumizi ya nishati safi ni ya gharama kubwa ikilinganishwa na nishati nyingine zinazotumika. “Nishati safi tunaihitaji sana, lakini tutaendelea kutumia nishati nyinginezo hususani kwa ajili ya upatikanaji wa umeme. Tunahitaji kuleta maendeleo na kubadili maisha ya wananchi wetu,” alihitimisha Dk. Biteko.
Share This Story, Choose Your Platform!
continue reading
Related Posts
DODOMA: Kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini […]
Mkurugenzi wa Taasisi ya HakiRasilimali Adam Anthony “Wananchi wanapaswa kufurahia […]