Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) Shirika la Wanawake katika shughuli za uziduaji (WIMO), Lightness Salema, ameishauri serikali kuweka utaratibu wa kuwapatia ujuzi wataalam wa ndani, kwa lengo la kuongeza mnyororo wa thamani katika sekta ya madini. Ametoa rai hiyo leo Novemba 9,2023 wakati wa mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Uziduaji lililofanyika mkoani Dodoma, akasema: Ili kuhakikisha ujuzi unabaki kuwa faida ya Tanzania, wataalamu hao wapelekwe nje ya nchi kuingeza maarifa kwa maeneo mbalimbali, ikiwemo ukataji vito na uchorongaji miamba, lakini wawekewe utaratibu utakaowalazimu kurudi nchini, na sio kulowea kwa kutumikia na kunufaisha mataifa mengine. “Na kikubwa tuangalie vipaji na uwezo wa watanzania. Sio lazima anayepelekwa nje ya nchi awe na elimu ya juu. Kwa mfano, ukiangalia mtu anayekata vito vya thamani nchini India, hana hata shahada ya kwanza,” amesema.

Share This Story, Choose Your Platform!

continue reading

Related Posts