Afshin Nazir, Afisa sera na uchechemzi wa AFRODAD: “Afrika ni bara tajiri na masikini wakati huohuo tunazo rasilimali nyingi za kutufanya tuwe matajiri lakini bado tunaishi katika umasikini mkubwa” Nazir amesema sababu kubwa ya umasikini barani Afrika ni kukosekana kwa mikakati na usimamizi madhubuti wa rasilimali zilizopo. Amezungumzia athari za madeni katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi akisema changamoto ya madeni kwa nchi yanakwaza juhudi zote muhimu.
“Mataifa mengi ya Afrika yanatumia kiasi kikubwa cha mapato yake kulipa madeni kwa kuwa yanadaiwa fedha nyingi lakini tukiwa na mikakati mizuri tunaweza kutumia rasilimali zetu kugharimia mambo yote muhimu ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi” Vilevile amesema kutokana na kutokuwa na mikakati madubuti Afrika inakosa sauti katika majukwaa ya mabadiliko ya tabianchi duniani licha ya kuwa ni mdau namba moja katika safari hiyo.

Share This Story, Choose Your Platform!

continue reading

Related Posts